Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2025

SIKU YA SABATO NI IPI?

Wengi, wanatunza Siku ya jumapili na wengine Siku ya jumamosi... Swali linakuja je, Kati ya hizi mbili ipi ni Siku ya kweli?...  SABATO YA BWANA  Biblia inasema;  Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. [Waefeso 4:5] Kwa mujibu wa Biblia upo ubatizo mmoja(wa maji Mengi) Yuko Mungu mmoja na Imani moja.....(Siku ya ibada lazima iwe moja) Kama wakiwa na Imani moja....  SABATO NI AMRI YA NNE Katika kutoka 20:8-11 tunasoma maneno haya;  [8]Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.  [9]Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;  [10]lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.  [11]Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.  -----------------------------...

SHERIA YA MUNGU

 Kutoka mlima Sinai, Bwana mwenyewe aliandika sheria yake kwa Chanda chake mwenyewe.... Akiisha kuiandika alimkabidhi mtumishi wake Mussa, kupitia Sheria yake twaweza kuwa salamaa, kupitia Yesu atutegemezaye na kutupatia nguvu za kuenenda Kama sheria ilivyo!! [Kutoka 31:18] ----------------- JE, UNAMPENDA MUNGU?  Maandiko yanasema: Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. 1Yohana 2:4.  -- Sheria ya Mungu, ni maelekezo namna ya kuishi kwa yule aliyekombolewa kutoka kwenye utumwa wa dhambi....... Iwapo mtu huyo ataishi kinyume na maagizo hayo, ni dhahiri kuwa bado hajakombolewa, pili bado Hana utii kwa Bwana wake!...  AMRI KUMI ZA MUNGU Amri kumi za MUNGU tunazipata katika kitabu Cha kutoka 20:1-17  .............  Ziko katika mafungu mawili, ambayo ni  A)Amri ya 1-4 zinahusu upendo Kati ya mwanadamu na Mungu  B)Amri ya 5-10 zinahusu upendo Kati ya mwanadamu na mwanadamu mwenzake 1. AMRI YA KWANZA...