Kutoka mlima Sinai, Bwana mwenyewe aliandika sheria yake kwa Chanda chake mwenyewe.... Akiisha kuiandika alimkabidhi mtumishi wake Mussa, kupitia Sheria yake twaweza kuwa salamaa, kupitia Yesu atutegemezaye na kutupatia nguvu za kuenenda Kama sheria ilivyo!! [Kutoka 31:18]
-----------------
JE, UNAMPENDA MUNGU?
Maandiko yanasema:
Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. 1Yohana 2:4.
-- Sheria ya Mungu, ni maelekezo namna ya kuishi kwa yule aliyekombolewa kutoka kwenye utumwa wa dhambi....... Iwapo mtu huyo ataishi kinyume na maagizo hayo, ni dhahiri kuwa bado hajakombolewa, pili bado Hana utii kwa Bwana wake!...
AMRI KUMI ZA MUNGU
B)Amri ya 5-10 zinahusu upendo Kati ya mwanadamu na mwanadamu mwenzake
1. AMRI YA KWANZA
*[3]Usiwe na miungu mingine ila mimi*
2. AMRI YA PILI
[4]*Usijifanyie sanamu ya kuchonga*, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
[5]Usivisujudie wala kuvitumikia.......
3. AMRI YA TATU
*[7]Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako,* maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
--- kuapa, kulitumia mahakami kuthibitisha uongo... hapana!! Usilitumie kufanya uongo uonekane kuwa ni ukweli...
4. AMRI YA NNE
[8] *Ikumbuke siku ya Sabato uitakase*
[9]Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote
[10]lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako..........
5. AMRI YA TANO
*[12]Waheshimu baba yako na mama yako*; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako
6. AMRI YA SITA
*Usiue*
7. AMRI YA SABA
*[14]Usizini*
8. AMRI YA NANE
*[15]Usiibe*
9. AMRI YA TISA
*[16]Usimshuhudie jirani yako uongo*
10. AMRI YA KUMI
[17]Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako>> [kutoka 20:1-17]
=========================
Sheria ya Mungu, haikuishia msalabani, sheria ya Mungu itadumu milele;[math 5:17-18]
Maana dhambi ilikuja kwa sababu ya kuvunja sheria, ukiondoa sheria hakuna dhambi tena, je, NI kweli hakuna dhambi...hapana,
<<<<<Mkinipenda, mtazishika amri zangu..[Yoh 14:15]>>>>>>
...........................................
Amani ya Bwana iwe Juu yako---Hesabu 6:25
Comments
Post a Comment