Skip to main content

MTU ANAPOKUFA ANAENDA WAPI?

Mara nyingi, tumesikia hadithi nyingi kuhusu wafu, wengine wakiamini kuwa mtu anapokufa huwa anaendelea kuishi katika ulimwengu mwingine, je! Ukweli halisi ni upi?? 

Karibu tujifunze pamojaa kwa kuangalia maandiko yanasemaje!! 

MWANADAMU ALIUMBWA

Mwanadamu ni matokeo ya udongo jumlisha pumzi ya uhai, 
[Mwanadamu=udongo+pumzi ya uhai]

BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. (Mwanzo:2:7)

Hivyo, ukichukua udongo ukatoa na pumzi ya uhai unapata maiti, 
[Maiti=Udongo-pumzi ya uhai]

KIFO HAUKUWA MPANGO WA MUNGU

Kifo ni matokeo ya dhambi, baada ya adamu na Hawa kuvunja sheria ya Mungu, pale kwenye bustani ya Edeni[mwanzo 3:1-24]

Ikiwa Kama adamu na Hawa wasingetilia Shaka maagizo ya Mungu, Leo kifo kisingekuwepo kabisaa hakuna hata mmoja ambaye angekuwa anahisi maumivu tunayohisi leoo.... (EGW, Pendo lisilo kifani, sura ya Anguko la Mwanadamu)

Biblia inafananisha KIFO na usingizi, maana baada ya muda Yesu akirudi atawafufua watu wote....ni usingizi ambaye aliyelaa hawezi kujiamusha/kuamshwa, Wala hauna ndoto [Yohana 5:28]

WALIOKUFA WAKO WAPI HASA?

Agano la Kale linapaita mahali walipo wafu kuwa ni sheol (Kiebrania) na Agano Jipya hades (Kigiriki).
Katika Maandiko, maana rahisi ya sheol (kuzimu) ni kaburi. Maana ya hades ni sawa na maana ya sheol.

Wafu wote huenda mahali hapo(Zab.89:48), wema kwa waovu. 
Yakobo alisema atamshukia mwanawe hata kuzimu (Mwa.37:35).
Ardhi ilipofunguka, iliwameza Kora pamoja na wenzake hadi kwenye sheol (Hes.16:30).

1. Aliyekufa hajui neno lolote

Kwa mujibu wa maandiko, wale wanaoamini kuwa maiti huwa anaweza kuhisi maumivu, Kama sisi tulio hai.... Wanakosea! 

Mhubiri 9:5
[5]kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. 

2. Katika usingizi huo, hakuna kufikiri, au kutenda Kama aliye hai.

Kwa kuwa mawazo yake hupotea, hawezi kufikiri chochote! (Zab.146:4), (Qurani 12:106 ufafanuzi), Quran 35:22 

3. Aliyekufa hawezi kutokea Kama muzimu, au Kama roho 

Ikiwa aliyekufa hajui chochote je, mbona Mara nyingi tumetokewa na bibi, babu, ndugu, jamaa na marafiki kwenye ndoto hao ni akina Nani Kama wafu hawawezi kuzungumza nasi? 

Jibu: 2 Wakorintho 11:14.
 “Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.”

Anayekuja katika usingizi ....huwa sio Yeye maana aliyekufa hawezi ongea, Ila ni SHETANI anajigeuza na kuvaa uhusika wa rafiki, ndugu yako! Ili apate kukudanganya!....

Amewahi kufanya hivyo, ili kudanganya mfalme wa Israel, [1 Samweli 28:7–25]


YESU AKIJA ATAWAFUFUA WAFU WOTE! 

Biblia inasema: 
Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. (Daniel 12:2)

Hii inamanisha watakatifu na waovu wote...wako kaburini, YESU akija atawafufua kila mmoja alipwe sawa sawa na matendo yake!! 
.............................................................................

UKIMTUMAINI, UKIMWAMINI, NA KUMFATA YESU, UZIMA WA MILELE NI WAKO! 

Wanaomtumaini Yesu, hata wanapokufa wanakufa katika TUMAINI la kufufuliwa na kupata uzima wa milele... 

Yohana 6:39-40
[39]Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho. 

[40]Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 

Barikiwa Sana....
Amani ya Bwana iwe juu yako.. Hesabu 6:25


Comments

Popular posts from this blog

UHALISIA WA UWEPO WA MUNGU

 JE MUNGU YUPO KWELI?  Watu wengi wamehoji maswali Mengi ikiwa Mungu yupo au la, na baadhi wamefikia hatua ya kusema kuwa hakuna Mungu!  Swali linakuja ikiwa Mungu yupo wawezaje kuthibitisha Imani yako?  UTHIBITISHO WA  UWEPO WA MUNGU  Mungu, yupo! Upo uthibitisho tosha kujibu swali hili Kama ifuatavyo!.  1. Uwepo wa Ulimwengu huu  Vitu vinavyoonekana vyote, Kama vile mimea, wanyama, mfumo wa jua (Solar system) na sayari zingine zote, kuwepo kwake Lazima awepo mwasisi wake! Maana hakuna uthibitisho wowote unaonesha kuwa sayari yaweza jiumba yenyewe!!, Wala dhana ya uibukaji haileti mantiki kusema mfumo wa Jua ulivyokaa uliibuka tuu.  2.  Mpangilio, mwafaka na Muundo wa Ulimwengu.  Jinsi Ulimwengu ulivyo, Kuna aliyepangilia, aka design(Muundo) ili kupata rangi/mwonekano mzuri wenye kuvutia, angalia aina za mimea, maua, wanyama tofauti kwa aina zake, ndege tofauti wakivutia sana!  Jua litoke mashariki kwenda magharibi Bila kuhama...

SIKU YA SABATO NI IPI?

Wengi, wanatunza Siku ya jumapili na wengine Siku ya jumamosi... Swali linakuja je, Kati ya hizi mbili ipi ni Siku ya kweli?...  SABATO YA BWANA  Biblia inasema;  Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. [Waefeso 4:5] Kwa mujibu wa Biblia upo ubatizo mmoja(wa maji Mengi) Yuko Mungu mmoja na Imani moja.....(Siku ya ibada lazima iwe moja) Kama wakiwa na Imani moja....  SABATO NI AMRI YA NNE Katika kutoka 20:8-11 tunasoma maneno haya;  [8]Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.  [9]Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;  [10]lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.  [11]Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.  -----------------------------...