Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2025

UUMBAJI

 UUMBAJI WA SAYARI YETU YA DUNIA  Dunia yetu hii na vyote vilivyomo viliumbwa na Mungu kwa muda wa siku sita. Hapa ni siku sita za masaa 24HRS, (Yome[Hebrew]- inayotafasiliwa Kama siku...inamanisha tangu jua kuzama Hadi Jua kuzama sio miaka 6,000 Kama waanavyodhani wengine. [Mwanzo 1:1] Dunia Ina vitu vingi, ndiyo! Mimea aina tofauti, wanyama, n.k kwa Mungu haya sio Mengi kiasi Cha kushindwa kuumba kwa Siku sita tuu,  alikuwa anatamka vinatokea!! Kama ifuatavyo;   -- Siku ya kwanza (01) Siku ya kwanza Mungu aliumba *NURU*         hapo  ndipo mwanzo wa Giza na Nuru ulipopatikana.....  Mwanzo 1:3-5 [3]Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru...  -- Siku ya pili (02) Siku ya pili Mungu aliumba *ANGA*  Mwanzo 1:6-8  [6 ]Mungua akasema Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji....  -- Siku ya tatu (03)  Siku ya tatu Mungu aliumba, *NCHI KAVU* *BAHARI* na *MIMEA*  Mwanzo 1:9-11 [9]Mungu akasema,...

UHALISIA WA UWEPO WA MUNGU

 JE MUNGU YUPO KWELI?  Watu wengi wamehoji maswali Mengi ikiwa Mungu yupo au la, na baadhi wamefikia hatua ya kusema kuwa hakuna Mungu!  Swali linakuja ikiwa Mungu yupo wawezaje kuthibitisha Imani yako?  UTHIBITISHO WA  UWEPO WA MUNGU  Mungu, yupo! Upo uthibitisho tosha kujibu swali hili Kama ifuatavyo!.  1. Uwepo wa Ulimwengu huu  Vitu vinavyoonekana vyote, Kama vile mimea, wanyama, mfumo wa jua (Solar system) na sayari zingine zote, kuwepo kwake Lazima awepo mwasisi wake! Maana hakuna uthibitisho wowote unaonesha kuwa sayari yaweza jiumba yenyewe!!, Wala dhana ya uibukaji haileti mantiki kusema mfumo wa Jua ulivyokaa uliibuka tuu.  2.  Mpangilio, mwafaka na Muundo wa Ulimwengu.  Jinsi Ulimwengu ulivyo, Kuna aliyepangilia, aka design(Muundo) ili kupata rangi/mwonekano mzuri wenye kuvutia, angalia aina za mimea, maua, wanyama tofauti kwa aina zake, ndege tofauti wakivutia sana!  Jua litoke mashariki kwenda magharibi Bila kuhama...

KUHUSU MWANDISHI

Mmliki wa   blog hii anajulikana kwa jina la ANCENTY STANSALUSE, kijana kutoka nchini Tanzania,  Amehitimu shahada(degree) katika fani ya management ya uhandisi wa viwanda katika chuo kikuu mzumbe kilichoko nchini Tanzania, kampasi kuu mkoa wa morogoro!  Ni miongoni mwa wafuasi wa Yesu Kristo, mmoja Kati ya wanaotangaza ujio wa Yesu Kristo kwa Mara ya pili,  Blog hii ilianzishwa rasmi April, 24 2025, kwa lengo kuu moja tu, kuhubiri neno la Mungu mwenyezi, kufikisha ujumbe wa malaika watatu kwa njia ya mtandao (Digital evangelism)  Hivyo, kwa swali lolote linalokutatiza  usisite kuuliza! Maana tamanio letu ni wewe kujua kweli... # Wewe ni wa thamani kwetu, zaidi Sana mbele za MUNGU!!  --- Amani ya Bwana iwe Juu yako---                Hesabu: 6:25