Skip to main content

KUHUSU MWANDISHI

Mmliki wa  blog hii anajulikana kwa jina la ANCENTY STANSALUSE, kijana kutoka nchini Tanzania, 

Amehitimu shahada(degree) katika fani ya management ya uhandisi wa viwanda katika chuo kikuu mzumbe kilichoko nchini Tanzania, kampasi kuu mkoa wa morogoro! 

Ni miongoni mwa wafuasi wa Yesu Kristo, mmoja Kati ya wanaotangaza ujio wa Yesu Kristo kwa Mara ya pili, 

Blog hii ilianzishwa rasmi April, 24 2025, kwa lengo kuu moja tu, kuhubiri neno la Mungu mwenyezi, kufikisha ujumbe wa malaika watatu kwa njia ya mtandao (Digital evangelism) 

Hivyo, kwa swali lolote linalokutatiza  usisite kuuliza! Maana tamanio letu ni wewe kujua kweli...

#Wewe ni wa thamani kwetu, zaidi Sana mbele za MUNGU!! 

--- Amani ya Bwana iwe Juu yako---                Hesabu: 6:25 


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MTU ANAPOKUFA ANAENDA WAPI?

Mara nyingi, tumesikia hadithi nyingi kuhusu wafu, wengine wakiamini kuwa mtu anapokufa huwa anaendelea kuishi katika ulimwengu mwingine, je! Ukweli halisi ni upi??  Karibu tujifunze pamojaa kwa kuangalia maandiko yanasemaje!!  MWANADAMU ALIUMBWA Mwanadamu ni matokeo ya udongo jumlisha pumzi ya uhai,  [Mwanadamu=udongo+pumzi ya uhai] BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. (Mwanzo:2:7) Hivyo, ukichukua udongo ukatoa na pumzi ya uhai unapata maiti,  [Maiti=Udongo-pumzi ya uhai] KIFO HAUKUWA MPANGO WA MUNGU Kifo ni matokeo ya dhambi, baada ya adamu na Hawa kuvunja sheria ya Mungu, pale kwenye bustani ya Edeni[mwanzo 3:1-24] Ikiwa Kama adamu na Hawa wasingetilia Shaka maagizo ya Mungu, Leo kifo kisingekuwepo kabisaa hakuna hata mmoja ambaye angekuwa anahisi maumivu tunayohisi leoo.... (EGW, Pendo lisilo kifani, sura ya Anguko la Mwanadamu) Biblia inafananisha KIFO na usingizi, maana baada ya muda Yesu akirudi...

UHALISIA WA UWEPO WA MUNGU

 JE MUNGU YUPO KWELI?  Watu wengi wamehoji maswali Mengi ikiwa Mungu yupo au la, na baadhi wamefikia hatua ya kusema kuwa hakuna Mungu!  Swali linakuja ikiwa Mungu yupo wawezaje kuthibitisha Imani yako?  UTHIBITISHO WA  UWEPO WA MUNGU  Mungu, yupo! Upo uthibitisho tosha kujibu swali hili Kama ifuatavyo!.  1. Uwepo wa Ulimwengu huu  Vitu vinavyoonekana vyote, Kama vile mimea, wanyama, mfumo wa jua (Solar system) na sayari zingine zote, kuwepo kwake Lazima awepo mwasisi wake! Maana hakuna uthibitisho wowote unaonesha kuwa sayari yaweza jiumba yenyewe!!, Wala dhana ya uibukaji haileti mantiki kusema mfumo wa Jua ulivyokaa uliibuka tuu.  2.  Mpangilio, mwafaka na Muundo wa Ulimwengu.  Jinsi Ulimwengu ulivyo, Kuna aliyepangilia, aka design(Muundo) ili kupata rangi/mwonekano mzuri wenye kuvutia, angalia aina za mimea, maua, wanyama tofauti kwa aina zake, ndege tofauti wakivutia sana!  Jua litoke mashariki kwenda magharibi Bila kuhama...

SIKU YA SABATO NI IPI?

Wengi, wanatunza Siku ya jumapili na wengine Siku ya jumamosi... Swali linakuja je, Kati ya hizi mbili ipi ni Siku ya kweli?...  SABATO YA BWANA  Biblia inasema;  Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. [Waefeso 4:5] Kwa mujibu wa Biblia upo ubatizo mmoja(wa maji Mengi) Yuko Mungu mmoja na Imani moja.....(Siku ya ibada lazima iwe moja) Kama wakiwa na Imani moja....  SABATO NI AMRI YA NNE Katika kutoka 20:8-11 tunasoma maneno haya;  [8]Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.  [9]Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;  [10]lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.  [11]Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.  -----------------------------...