Katika somo la UUMBAJI, tuliona kuwa Mungu aliumba dunia ikiwa nzuri, yenye kuvutia Sana! Swali ni ikiwa hivi ndivyo, shida ilitokea wapi...? Maana Leo dunia imejaa magonjwa, huzuni, vilio, vifo, shida ilianzia EDENI, ADAM & HAWA EDENI Mwanzo 2:8-9, 2:16-17 [8]BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya [9]BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya. [16]BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula [17]walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika. ------ MTI WA UJUZI WA MEMA & MABAYA KAMA KIPIMO CHA UTII Katika kitabu Cha Ellen G White, Pendo lisilo kifani sura isemayo msiba, anasema!. ------- .....Mungu alichagua kuujaribu uaminifu...