Skip to main content

ANGUKO LA LUSIFA

 Mwandishi mmoja (Ellen G White)  katika kitabu chake Cha Pendo lisilo kifani(PLK) sura isemayo Uasi, anaandika maneno yafuatayo!


Lusifa alikuwa malaika mkuu

Kabla ya uasi wake mbinguni, Lusifa alikuwa malaika mkuu na aliyetukuka, ambaye kwa heshima, alikuwa akimfuatia Mwana wa Mungu(Yesu Kristo) 

Uso wake, kama zilivyokuwa za malaika wengine, ulikuwa ni wa upole ulioangaza furaha. Kipaji cha uso wake kilikuwa kimeinuka na kipana, kikionesha uwezo mkubwa wa kiakili......

Nuru ya pekee ilimulika kutoka katika uso wake ikiangaza kumzunguka kwa uangavu na uzuri kuliko ilivyokuwa kwa malaika wengine [EGW, PLK 5.1] 

Uzuri wake lusifa, ulimfanya awe na kiburi

Mungu alikuwa amempa cheo cha juu, lakini hilo halikumfanya arejeshe shukrani na sifa kwa Muumba wake. 

Alitamani kufikia kimo cha Mungu mwenyewe....

Aliona fahari kwa sababu ya hadhi yake iliyotukuka. Alijua kuwa alikuwa anaheshimiwa na malaika....

Alikuwa amepata fursa ya kuwa karibu na Muumbaji mkuu, na miale ya daima ya nuru tukufu iliyomzunguka Mungu wa milele kwa namna ya pekee iliangaza juu yake. 

Alifikiria jinsi ambavyo malaika walitii amri zake kwa haraka na furaha. Je mavazi yake hayakuwa nuru na ya kupendeza? Kwa nini Kristo(Yesu)  aheshimiwe kiasi kile badala yake? - EGW, PLK 5.2

_-_-_-_-_-_-_-

BWANA alimuumba lusifa kwa namna ya ajabu Sana, maana aliumbwa kwa Vito vya thamani.. akiki, yakuti manjano, almasi, n.k  [Ezekiel 28:13]

Lusifa aliangusha jeshi kubwa la malaika 

Kwa sababu ya uzuri wake, akaanza kutamani nafasi ya Mungu, BWANA alimpatia nafasi ya kutubu lakini, hakuitumia vizuri, taratibu akawashawishi ¹/3 ya jeshi la malaika wa mbinguni wakawa upande wake, hao ndo wanaitwa leo (Mapepo na Majini) akawaahidi kuwa baada ya kumpindua Mungu, atatengeneza serikali Bora kuliko ya Mungu, ambayo kwayo kila mmoja ataweza kufanya atakavyo! 

Lusifa kuondolewa mbinguni

Kwakuwa  Yeye lusifa ni kiumbe, kamwe asingeweza kumpindua Mungu, BWANA kwa upendo wake alivyoona Lusifa hajafanya Toba ya dhati akaamua kumfukuza Yeye na jeshi lake watoke mbinguni....ili kila mmoja aone uovu uliokuwa umefichika ndani yake, ndo maana hakumwangamiza kwa muda huo... [Ezekiel 23:17], pia Soma [Ufunuo 12:7-9]

Shetani alipoondolewa mbinguni, aliwatuma malaika wake wakaangalie katika sayari zingine ikiwa itapatikana nafsi waingie, Ila walikosa katika sayari zingine.....mwisho wa siku wakabahatika kupata nafasi katika sayari hii ya dunia. 

_-_-_-_-_-_-_-_-_--_-_-_-_-_-_--_-_-_-_-_-_-_-_--_-_-_


Toka lusifa Hadi kuitwa Shetani

Kuanzia hapo jina lake likabadilika kutoka kuitwa LUSIFA(Nyota ya Asubuhi) mbeba Nuru Hadi kuitwa SHETANI, IBILIS (Mshitaki, mpinzani, au adui) EGW, PLK 7.3 

Hadi leo shetani Yupo, na Hukumu yake ni kuangamizwa kwa Moto wa milele Siku ya Hukumu ikifika, Hana nafasi ya kutubu Tena!! Anachokifanya ni kukusanya wafuasi ili Siku ya mwisho apotee na idadi kubwa!! 

====================================

Ila usiogope, Mungu ameweka nafasi ya kukuokoa! Ikiwa unatamani kukwepa adui huyu mkuu.... 

Karibu SoMo linalofuata [Anguko la Mwanadamu] 


----Amani ya Bwana iwe Juu yako---              Hesabu 6:25 
















Comments

Popular posts from this blog

MTU ANAPOKUFA ANAENDA WAPI?

Mara nyingi, tumesikia hadithi nyingi kuhusu wafu, wengine wakiamini kuwa mtu anapokufa huwa anaendelea kuishi katika ulimwengu mwingine, je! Ukweli halisi ni upi??  Karibu tujifunze pamojaa kwa kuangalia maandiko yanasemaje!!  MWANADAMU ALIUMBWA Mwanadamu ni matokeo ya udongo jumlisha pumzi ya uhai,  [Mwanadamu=udongo+pumzi ya uhai] BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. (Mwanzo:2:7) Hivyo, ukichukua udongo ukatoa na pumzi ya uhai unapata maiti,  [Maiti=Udongo-pumzi ya uhai] KIFO HAUKUWA MPANGO WA MUNGU Kifo ni matokeo ya dhambi, baada ya adamu na Hawa kuvunja sheria ya Mungu, pale kwenye bustani ya Edeni[mwanzo 3:1-24] Ikiwa Kama adamu na Hawa wasingetilia Shaka maagizo ya Mungu, Leo kifo kisingekuwepo kabisaa hakuna hata mmoja ambaye angekuwa anahisi maumivu tunayohisi leoo.... (EGW, Pendo lisilo kifani, sura ya Anguko la Mwanadamu) Biblia inafananisha KIFO na usingizi, maana baada ya muda Yesu akirudi...

UHALISIA WA UWEPO WA MUNGU

 JE MUNGU YUPO KWELI?  Watu wengi wamehoji maswali Mengi ikiwa Mungu yupo au la, na baadhi wamefikia hatua ya kusema kuwa hakuna Mungu!  Swali linakuja ikiwa Mungu yupo wawezaje kuthibitisha Imani yako?  UTHIBITISHO WA  UWEPO WA MUNGU  Mungu, yupo! Upo uthibitisho tosha kujibu swali hili Kama ifuatavyo!.  1. Uwepo wa Ulimwengu huu  Vitu vinavyoonekana vyote, Kama vile mimea, wanyama, mfumo wa jua (Solar system) na sayari zingine zote, kuwepo kwake Lazima awepo mwasisi wake! Maana hakuna uthibitisho wowote unaonesha kuwa sayari yaweza jiumba yenyewe!!, Wala dhana ya uibukaji haileti mantiki kusema mfumo wa Jua ulivyokaa uliibuka tuu.  2.  Mpangilio, mwafaka na Muundo wa Ulimwengu.  Jinsi Ulimwengu ulivyo, Kuna aliyepangilia, aka design(Muundo) ili kupata rangi/mwonekano mzuri wenye kuvutia, angalia aina za mimea, maua, wanyama tofauti kwa aina zake, ndege tofauti wakivutia sana!  Jua litoke mashariki kwenda magharibi Bila kuhama...

SIKU YA SABATO NI IPI?

Wengi, wanatunza Siku ya jumapili na wengine Siku ya jumamosi... Swali linakuja je, Kati ya hizi mbili ipi ni Siku ya kweli?...  SABATO YA BWANA  Biblia inasema;  Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. [Waefeso 4:5] Kwa mujibu wa Biblia upo ubatizo mmoja(wa maji Mengi) Yuko Mungu mmoja na Imani moja.....(Siku ya ibada lazima iwe moja) Kama wakiwa na Imani moja....  SABATO NI AMRI YA NNE Katika kutoka 20:8-11 tunasoma maneno haya;  [8]Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.  [9]Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;  [10]lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.  [11]Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.  -----------------------------...