Katika somo la UUMBAJI, tuliona kuwa Mungu aliumba dunia ikiwa nzuri, yenye kuvutia Sana!
Swali ni ikiwa hivi ndivyo, shida ilitokea wapi...? Maana Leo dunia imejaa magonjwa, huzuni, vilio, vifo, shida ilianzia EDENI,
ADAM & HAWA EDENI
Mwanzo 2:8-9, 2:16-17
[8]BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya
[9]BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
[16]BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula
[17]walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
------
MTI WA UJUZI WA MEMA & MABAYA KAMA KIPIMO CHA UTII
Katika kitabu Cha Ellen G White, Pendo lisilo kifani sura isemayo msiba, anasema!.
-------
.....Mungu alichagua kuujaribu uaminifu wao kabla hajawafanya kuwa salama milele. Shetani aliruhusiwa kuwajaribu. Iwapo wangelishinda jaribu lile, wangepata kibali cha Mungu na malaika wa mbinguni milele zote. - PLK 14.2
----Mungu, alitaka kupima uaminifu wao, Shetani alikuja kwa Umbo la nyoka, Kisha hichi ndicho alicho fanya!!---
HAWA ALIDANGANYWA
Mwanzo 3:1-4
[1]Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
[2]Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
[3]lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
[4]Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa!
===============================
Shetani katika Umbo la nyoka, akisha kumshawishi, Hawa! Kwa huzuni, Hawa akashawishika! ✍️
Biblia inasema:
Mwanzo 3:6
[6]Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
HUKUMU YA MUNGU EDENI
Baada ya wawili Hawa, kutilia Shaka maagizo ya Mungu na kufuata uongo wa shetani, wakawa wamevunja Sheria ya YEHOVA!!
Mungu alipowatembelea kuwatafuta(ilikuwa kawaida ya MUNGU kuwatembelea) wakaanza, kujificha! akisha kuhojiana nao, akahitimisha kwa kuilaani ardhi, nyoka, na kuwatangazia madhara yatakayowapata baada ya kuvunja agizo lake! [Mwanzo 3:8-19]
-----------------------------------------------
Kuanzia hapo dhambi ikaingia, kifo kikaingia, magonjwa, shida, mateso! Mwanadamu akawa ameanguka! Kwa kuvunja maagizo ya Mungu!! ✍️
=============
Pamoja na Adam na Hawa kuvunja maagizo ya Mungu, Mungu aliandaa mpango wa kuwatoa katika shimo la dhambi, SoMo linalofuata! Tutajifunza Juu suluhisho baada ya Anguko.......
----Amani ya Bwana iwe Juu yako---. Hesabu 6:25.
Comments
Post a Comment