SoMo lililopita tuliona kuwa ukimwamini Yesu, ukatubu utasamehewa dhambi, hata Kama zilikuwa nyingi kiasi gani....upendo mkuu ajabu! Kiroho mtu aweza kuzaliwa Mara ya pili kwa njia ya ubatizo!......
Kwa njia ya ubatizo, mtu atamkiri Yesu, kuwa ni mwokozi wake, ndiyo njia Mungu aliyoiweka ya kutuvusha kutoka mahali pa dhambi, kutuunganisha na Mwokozi, kwa kufanya tendo hili...inakuwa umemkubali Yesu waziwazi.... hivyo, baada ya kubatizwa atakupokea, Kama mtoto wake!....nawe utakuwa umeanza safari mpya ya maisha!
UBATIZO
Je, mtu anayebatizwa anapaswa awe na sifa gani?
Biblia inasema:
Marko 16:15-16
[15]Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
[16]Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
Kutoka kwenye Aya hii tunapata Mambo 3.
a) Injili
Kabla mtu hajabatizwa lazima ajue kweli (Neno la Mungu), ili aelewe anabatizwa kwa sababu gani!.
b)Imani
Baada ya kuhubiriwa, na kuitikia sauti ya Roho mtakatifu, ataamini ya kuwa aliyofundishwa ni kweli, hii ni hatua ya pili, hawezi amini Bila kufundishwa!
c) Ubatizo
Baada ya kufundishwa, na kuamini, hatua ya mwisho atafanya uamuzi wa kuyatoa maisha yake kwa mwokozi kwa njia ya ubatizo!.
Zingatia:
Mtoto mdogo hawezi batizwa, maana hizi hatua tatu haziendani na Yeye! Hawezi elewa, hawezi amini...mpaka akifikia umri wa kujitambuaa ndipo aweza kubatizwa!
-----------------------------------
-----------------------------------
-----------------------------------
UBATIZO SAHIHI NI UPI?
Kuna batizo za aina nyingi hapa duniani....je, katika hizo upi ni ubatizo sahihi unaotakiwa? Ambao unakubalika mbele ya Mungu mwenyezi?
Biblia inasema:
Waefeso 4:5
Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja
Kwa mujibu wa Biblia ubatizo upo mmoja tuu! Nao sio mwingine ni ule alionesha Yesu kristo mwenye kuanzisha Imani yetu!
*YESU ALIBATIZWA KWA MAJI MENGI*
Mathayo 3:13-16
[16]Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake
--------------------------
Hivyo, ubatizo sahihi unaotakiwa ni ubatizo aliobatizwa Yesu!
Biblia inasema:
1 Yohana 2:6
Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda
Maana ya Neno Ubatizo:
Neno Batiza ni neno la kiyunani (Baptizo) lenye maana ya *zamisha* tosa*
Huwezi zama, ndani ya maji ya bakuri, huwezi zama ndani ya Moto, Ila ndani ya maji Mengi unaweza kuzamishwa!
MAANA HALISI YA UBATIZO##
Kubatizwa ndani ya maji Mengi Kama alivyo fanya mwokozi Kuna Manisha Mambo yafuatayo!
I)Kuzika dhambi,
II)kufa pamoja na Mwokozi
II)kufufuka pamoja na Yesu, ukiwa kiumbe kipya!
[Warumi 6:1-4]
=====================
=====================
=====================
Kama umetambua ya kwamba Mungu ndiye muumbaji, naye anakupenda hata kumtoa mwanae wa pekee ili usiangamie, ameweka ubatizo Kama njia ya kuwapokea wote wanaitikia upendo wake! Je, unaweza kuwa miongoni mwao?? Usiogope unaweza!
-----Amani ya Bwana iwe Juu yako--- Hesabu 6:25
Comments
Post a Comment