Skip to main content

SULUHISHO BAADA YA ANGUKO

 HUZUNI ILIJAZA MBINGU

Huzuni iliijaza mbingu, pale wote walipotambua kuwa wanadamu walikuwa wamepotea na dunia ambayo Mungu alikuwa ameiumba ilikuwa ijazwe na wanadamu wapatikanao na mauti wanaopitia maisha ya taabu, maradhi, na mauti, pasipo na njia ya kuokoka kwa mkosaji. Familia yote ya Adamu ni lazima wafe. - EGW, PLK 26.1

MPANGO WA KUMKOMBOA MWANADAMU 

Ndipo Yesu akawafahamisha jeshi la malaika kwamba njia ya kuokoka ilikwisha kupatikana kwa ajili ya wanadamu waliopotea. - EGW, PLK 26.2

Aliwaambia kuwa alikuwa amemsihi Baba yake kwamba Yesu ajitolee maisha yake kuwa fidia ya kuwakomboa - EGW, PLK 26.2

Angetumikia adhabu ya kifo juu yake mwenyewe, ili kwa kupitia kwake wanadamu waweze kupata msamaha. -  EGW,PLK 26.2

YESU KATIKA UMBO LA BINADAMU

Angeacha utukufu wake wote mbinguni, na kutokea duniani kama mwanadamu, kujinyenyekesha kama mwanadamu, kupitia uzoefu wake mwenyewe ajue majaribu mbalimbali ambayo yangewapata wanadamu, ili apate kujua jinsi ya kuwasaidia wale ambao wangejaribiwa - EGW, PLK 26.3, [Filipi 2:5-8] 

Baada ya Mpango kuwekwa Yesu aliamua kuja duniani, kupitia tumbo la bikira mariam, akazaliwa Kama mtoto mchanga, akiisha kukua alianza kuhubiri neno la uzima [Mathayo 1:18-23] 

KIFO CHA YESU MSALABANI 

Hatimaye, baada ya kazi yake kama mwalimu kukamilishwa, angekabidhiwa katika mikono ya watu waovu na kustahimili karibu kila aina ya ukatili na maumivu ambayo Shetani pamoja na malaika zake wangeweza kuwachochea watu waovu kutenda - EGW, PLK 26.3

Mnamo mwaka wa 31 AD Siku ya ijumaa, Yesu alisulubishwa msalabani na Ijumaa jion, alizikwa kaburini, Kisha ilipofika jumapili Asubuhi alifufuka! [Luka 23:52-56, Luka 24:1-6] 


KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA 

Mwanadamu alipovunja Sheria ya Mungu (SoMo: ANGUKO LA MWANADAMU) ilikuwa afe milele, Yesu akatoa fidia, akafa badala yake mwanadamu, hivyo kupitia kwake Yesu uzima wa milele unapatikana, nafasi iliyokuwa imepotezwa Imerejea tena!! 
Soma [Isaya 53:1-12]. 


Unataka kuiona Mbingu? Imekupasa kumwamini YESU Kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako,Kisha jitoe kwake, maana alikufa kwa ajili yako-- 
============================
Biblia inasema: 
Yohana 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 

============================
Bwana kwa upendo wake, ametupatia nafasi ya pili, na iwapo hii Itapuuza haitakuwepo nafasi nyingine Tena!! 
Je, tutaipuuza nafasi hii Tena, ambayo imegharimu maisha ya mwokozi aliyekubali kufa kwa ajili yangu na wewe?? 

-------------------
----Amani ya Bwana iwe Juu yako--.                   Hesabu 6:25 

Comments

Popular posts from this blog

MTU ANAPOKUFA ANAENDA WAPI?

Mara nyingi, tumesikia hadithi nyingi kuhusu wafu, wengine wakiamini kuwa mtu anapokufa huwa anaendelea kuishi katika ulimwengu mwingine, je! Ukweli halisi ni upi??  Karibu tujifunze pamojaa kwa kuangalia maandiko yanasemaje!!  MWANADAMU ALIUMBWA Mwanadamu ni matokeo ya udongo jumlisha pumzi ya uhai,  [Mwanadamu=udongo+pumzi ya uhai] BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. (Mwanzo:2:7) Hivyo, ukichukua udongo ukatoa na pumzi ya uhai unapata maiti,  [Maiti=Udongo-pumzi ya uhai] KIFO HAUKUWA MPANGO WA MUNGU Kifo ni matokeo ya dhambi, baada ya adamu na Hawa kuvunja sheria ya Mungu, pale kwenye bustani ya Edeni[mwanzo 3:1-24] Ikiwa Kama adamu na Hawa wasingetilia Shaka maagizo ya Mungu, Leo kifo kisingekuwepo kabisaa hakuna hata mmoja ambaye angekuwa anahisi maumivu tunayohisi leoo.... (EGW, Pendo lisilo kifani, sura ya Anguko la Mwanadamu) Biblia inafananisha KIFO na usingizi, maana baada ya muda Yesu akirudi...

UHALISIA WA UWEPO WA MUNGU

 JE MUNGU YUPO KWELI?  Watu wengi wamehoji maswali Mengi ikiwa Mungu yupo au la, na baadhi wamefikia hatua ya kusema kuwa hakuna Mungu!  Swali linakuja ikiwa Mungu yupo wawezaje kuthibitisha Imani yako?  UTHIBITISHO WA  UWEPO WA MUNGU  Mungu, yupo! Upo uthibitisho tosha kujibu swali hili Kama ifuatavyo!.  1. Uwepo wa Ulimwengu huu  Vitu vinavyoonekana vyote, Kama vile mimea, wanyama, mfumo wa jua (Solar system) na sayari zingine zote, kuwepo kwake Lazima awepo mwasisi wake! Maana hakuna uthibitisho wowote unaonesha kuwa sayari yaweza jiumba yenyewe!!, Wala dhana ya uibukaji haileti mantiki kusema mfumo wa Jua ulivyokaa uliibuka tuu.  2.  Mpangilio, mwafaka na Muundo wa Ulimwengu.  Jinsi Ulimwengu ulivyo, Kuna aliyepangilia, aka design(Muundo) ili kupata rangi/mwonekano mzuri wenye kuvutia, angalia aina za mimea, maua, wanyama tofauti kwa aina zake, ndege tofauti wakivutia sana!  Jua litoke mashariki kwenda magharibi Bila kuhama...

SIKU YA SABATO NI IPI?

Wengi, wanatunza Siku ya jumapili na wengine Siku ya jumamosi... Swali linakuja je, Kati ya hizi mbili ipi ni Siku ya kweli?...  SABATO YA BWANA  Biblia inasema;  Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. [Waefeso 4:5] Kwa mujibu wa Biblia upo ubatizo mmoja(wa maji Mengi) Yuko Mungu mmoja na Imani moja.....(Siku ya ibada lazima iwe moja) Kama wakiwa na Imani moja....  SABATO NI AMRI YA NNE Katika kutoka 20:8-11 tunasoma maneno haya;  [8]Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.  [9]Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;  [10]lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.  [11]Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.  -----------------------------...