Uzoefu wa wokovu hujumuisha kutubu, kuungama, msamaha, kuhesabiwa haki na kutakaswa.
Mchakato huu huanza baada ya mwanadamu aliyeanguka dhambini kusikia wito ndani yake, ambao kimsingi ni sauti ya Roho mtakatifu inayonong'ona ndani yake, hivyo huanza kutambua dhambi yake na kuijutia.... ikiwa atakubali wito huo, hufanya uamuzi wa kufata hatua hizi, kutubu, kuungama , msamaha, kuhesabiwa haki na hatimaye hupata utakaso!![Matendo 2:37-38]
1.KUTUBU(TOBA)
Neno *kutubu / toba*, hutokana na neno la Kiebrania *nachum* lenye maana ya kuhuzunika, kusikitika.
Neno la Kigiriki lenye maana sawa na hilo ni *metanoeo*, lenye maaana ya kubadilisha mawazo/nia-
Hivyo, aliyetenda dhambi baada ya kutambua dhambi yake, husikitika kwa kufanya hivyo, Kisha hunuia kuiacha! Na kubadilisha mwelekeo wake! Huku ndiko kutubu!!
2. KUUNGAMA
Kuungama ni kukiri au kukubali Jambo wazi wazi Bila kusema uongo!
Aliyetenda dhambi baada ya kugundua kosa lake, hatua ya pili ni kuungama kwa Mungu, kuungama kwa mwanadamu mwenzakoo ni makosa, kwani naye pia ni mdhambi...[Mathayo 6:6]
Biblia inasema:
Isaya 1:18
Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
----------------------
Bwana ni mwaminifu hata Kama dhambi zetu ni nyingi kiasi gani, tukiungama kwa dhati tutasamehewa!!
3.KUHESABIWA HAKI
Baada ya kuungama utapokea msamaha, baada ya kupokea msamaha, Bwana atakuhesabia haki kupitia kwake Yesu.
Utahesabiwa kuwa huna hatia Tena!...sio kwa sababu ya matendo yako, Ila kwa kumwamini YESU na kutegemea haki yake, huku ukikiri kutostahili kwako..[1 kor 5:21]
Baada ya kuhesabiwa haki ya Yesu, matokeo yake ni Kama ifuatavyo:
A) Utakaso
Neno kutakaswa humaanisha kufanywa mtakatifu.
Toba ya kweli na kuhesabiwa haki huongoza kwenye kutakaswa, utakaso nayo ni kazi ya neema ya Mungu.
Hatua tatu za kutakaswa zinazofundishwa na Biblia ni:
(i) ni jambo lililokwisha kutimizwa
(ii) ni jambo linaloendelea kutimizwa sasa katika maisha ya mkristo
(iii) ni jambo litakalokamilishwa Yesu akirudi Mara ya pili.
Kwa wakati uliopita, wakati mtu anapohesabiwa haki, pia huwa amepokea utakaso kwa jina la Bwana Yesu [(1Kor. 6:11 cf. Yoh. 15:3)]
Kama matokeo ya kuitwa na Mungu [Rum. 1:7] waumini huitwa watakatifu kwa kuwa wako katika Kristo [(Wafil. 1:1, Yoh. 15:1-7)]
B) Kufanywa watoto wa Mungu.
Wakati huo huo tunapokea Roho ya kufanywa wana na warithi pamoja na Yesu [Rum. 8:15-17] Ni fursa bora kiasi gani, raha iliyoje?
C)Kuthibitishiwa wokovu.
Kuhesabiwa haki kunatuthibitishia kuwa ukombozi wetu ni hakika [Efe. 1:7]
D)Mwanzo wa maisha mapya ya ushindi.
Maisha yake aliyetaswa yanakuwa tofauti kabisa, na ya Mwanzo maana tabia na makando kando yote yameachwa!! Ndani yake hujaa furaha, huku akingojea ahadi ya mwokozi wake!.
E)Zawadi ya Uzima wa Milele.
Mahusiano yetu mapya na Yesu hutupatia zawadi ya uzima wa milele. Aliye na mwana ana uzima wa milele, asiye na mwana hana uzima [1Yoh. 5:12]
-----------
Baada ya kuishi maisha ya ushindi, washindi watazawadiwa taji ya uzima, watarithi nchi mpya, na kupewa maisha yasio na dhambi Tena, ni furaha ajabu!! Tena isiyoelezeka kufika hapa!!.......
====================
Barikiwa Sana,
----Amani ya Bwana iwe Juu yako--- Hesabu6:25
Comments
Post a Comment