Skip to main content

SIKU YA SABATO NI IPI?

Wengi, wanatunza Siku ya jumapili na wengine Siku ya jumamosi... Swali linakuja je, Kati ya hizi mbili ipi ni Siku ya kweli?... 

SABATO YA BWANA 

Biblia inasema; 
Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.
[Waefeso 4:5]
Kwa mujibu wa Biblia upo ubatizo mmoja(wa maji Mengi) Yuko Mungu mmoja na Imani moja.....(Siku ya ibada lazima iwe moja) Kama wakiwa na Imani moja.... 

SABATO NI AMRI YA NNE

Katika kutoka 20:8-11 tunasoma maneno haya; 
[8]Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 
[9]Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 
[10]lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 
[11]Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. 
---------------------------------
Hapa tunapata Mambo yafuatayo: 
#Sabato itunzwe
#Sabato hutunzwa Siku ya Saba ya juma 
#Sabato ni ya Bwana 
#Sabato imetakaswa, imebarikiwa, 
#Baada ya uumbaji Bwana aliacha kazi na kupumzika Siku hiyo. 

SABATO NI LINI LEO? 

Neno "sabato", Ina maana ya pumziko(rest) Siku hiyo mwanadamu anapaswa kupumzika, asifanye kazi yoyote (kutoka 20:10) Ila isipokuwa ibada tuu... ni Siku ya kufakari Mambo ya Mungu. 

Kutoka 20:10 inasema sabato ni Siku ya Saba...swali je, hiyo Siku ya Saba ni lini kwenye Siku zetu hizi leo?? 
=====
Biblia inasema:
Luka 24:1-3
[1]Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari. 
[2]Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi,
[3]Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu

Kwa mujibu wa Biblia Yesu alifufuka Siku ya 1 ya juma, ambayo Leo ndo jumapili, 

"Kama tukihesabia jumapili(Siku ya kwanza) aliyofufuka Yesu, jumatatu itakuwa Siku ya pili......"jumamosi" itakuwa Siku ya Saba"

Hivyo, kutoka 20 inasema Siku ya Saba ni sabato ya Bwana, akimanisha jumamosi ni sabato ya Bwana, hivyo! Siku ya jumamosi ndo Siku ya sabato-- ya Bwana. 

Jumamosi mwanadamu imempasa kupumzika na kuacha kazi zake, na kuutafuta Uso wa Bwana maana ni Siku ya sabato-- ya Bwana. 

MADHARA YA KUVUNJA SABATO 

Biblia inasema: 
Yakobo 2:10
Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
Kwa mujibu wa maandiko, ukivunja Amri ya Nne(sabato) ni sawa na yule ambaye hashiki Amri za MUNGU.....hivyo, Hukumu yake ni sawa na ya yule afanyae wizi, uzinzi....na maovu mengine. 

JE, SABATO ILIISHIA MSALABANI? 

Kujibu swali hili, zingatia haya; 
##Sabato itadumu milele, Isaya 66:22-23
##Yesu alitunza sabato, Luka 4:16 
##Mitume walitunza Sabato, Matendo 16:13
##Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu Marko 2:27. 
==================================================================================================================
Kwa hiyo, Sabato haikuishia msalabani,,,,maana hata baada ya Yesu kupaa mbinguni mitume waliendelea kuitunza!! 

Karibu, SoMo lijalo...tutaangalia nini kilitokea Hadi leo wengi wanashika jumapili
ambayo sio agizo la Mungu kabisaa! 

----Amani ya Bwana iwe juu yako Hesabu 6:24----- 

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MTU ANAPOKUFA ANAENDA WAPI?

Mara nyingi, tumesikia hadithi nyingi kuhusu wafu, wengine wakiamini kuwa mtu anapokufa huwa anaendelea kuishi katika ulimwengu mwingine, je! Ukweli halisi ni upi??  Karibu tujifunze pamojaa kwa kuangalia maandiko yanasemaje!!  MWANADAMU ALIUMBWA Mwanadamu ni matokeo ya udongo jumlisha pumzi ya uhai,  [Mwanadamu=udongo+pumzi ya uhai] BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. (Mwanzo:2:7) Hivyo, ukichukua udongo ukatoa na pumzi ya uhai unapata maiti,  [Maiti=Udongo-pumzi ya uhai] KIFO HAUKUWA MPANGO WA MUNGU Kifo ni matokeo ya dhambi, baada ya adamu na Hawa kuvunja sheria ya Mungu, pale kwenye bustani ya Edeni[mwanzo 3:1-24] Ikiwa Kama adamu na Hawa wasingetilia Shaka maagizo ya Mungu, Leo kifo kisingekuwepo kabisaa hakuna hata mmoja ambaye angekuwa anahisi maumivu tunayohisi leoo.... (EGW, Pendo lisilo kifani, sura ya Anguko la Mwanadamu) Biblia inafananisha KIFO na usingizi, maana baada ya muda Yesu akirudi...

UHALISIA WA UWEPO WA MUNGU

 JE MUNGU YUPO KWELI?  Watu wengi wamehoji maswali Mengi ikiwa Mungu yupo au la, na baadhi wamefikia hatua ya kusema kuwa hakuna Mungu!  Swali linakuja ikiwa Mungu yupo wawezaje kuthibitisha Imani yako?  UTHIBITISHO WA  UWEPO WA MUNGU  Mungu, yupo! Upo uthibitisho tosha kujibu swali hili Kama ifuatavyo!.  1. Uwepo wa Ulimwengu huu  Vitu vinavyoonekana vyote, Kama vile mimea, wanyama, mfumo wa jua (Solar system) na sayari zingine zote, kuwepo kwake Lazima awepo mwasisi wake! Maana hakuna uthibitisho wowote unaonesha kuwa sayari yaweza jiumba yenyewe!!, Wala dhana ya uibukaji haileti mantiki kusema mfumo wa Jua ulivyokaa uliibuka tuu.  2.  Mpangilio, mwafaka na Muundo wa Ulimwengu.  Jinsi Ulimwengu ulivyo, Kuna aliyepangilia, aka design(Muundo) ili kupata rangi/mwonekano mzuri wenye kuvutia, angalia aina za mimea, maua, wanyama tofauti kwa aina zake, ndege tofauti wakivutia sana!  Jua litoke mashariki kwenda magharibi Bila kuhama...