Skip to main content

KWANINI WENGI WANASALI JUMAPILI?

 Hili limekuwa swali kuu, kwanini idadi kubwa ya watu wanashika Siku ya kwanza(01) ya juma yaani jumapili Kama Siku ya ibada? 

Katika Somo la Siku ya sabato ni ipi tumejifunza, kuwa sabato ya kweli ni jumamos: 

Ikiwa ndivyo, jumapili iliingiaje Kama Siku ya ibada, hadi wengi wanaishika leoo...karibu tujifunze pamoja.... 

*YESU ALITUNZA SABATO*

Katika kitabu Cha Luka 4:16 anasema: ilikuwa desturi ya Mwokozi kusali Siku ya sabato(jumamosi) kumbe Yesu hakutunza jumapili Kama Siku ya ibada .... 

*MITUME WALITUNZA SABATO* 

Katika kitabu Cha matendo 16:13 neno linasema: Mitume hata baada ya Yesu kupaa mbinguni bado waliendelea kutunza sabato .....kamwe hawakushika jumapili, maana ilikuwa Siku ya kazi. 

*BADILIKO LA SABATO, LILITABIRIWA KWENYE MAANDIKO

Katika kitabu Cha Daniel 7:25 inasema:

[25]Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. 

Biblia, ilikwisha andika kuwa ufalme wa Nne uliozungumzwa katika Daniel sura ya 7, ambao ni Dora Rumi; ungefanya mambo haya, 
a)kubadili majira 
b)Kubadili Sheria ya Mungu, (Dan 7:25)
c)kuwatesa watakatifu wa Mungu kwa muda wa Miaka 3 na nusu sawa na Miaka 1260 
N:B 
👉Siku moja=mwaka 1, (Ezekiel 4:5)
👉Nyakati ni Aramaic words inamanisha mwaka,
👉Kibiblia mwezi una Siku 30, mwaka utakuwa na Siku (360days)
👉Hivyo,(nyakati 3.5 au 3.5years *360days= 1260days 
Kwa mujibu wa Ezekiel Siku 1260=Miaka 1260* 
*****************************
Historia iko wazi Dora ya kirumi ilitesa wakristo kuanzia mwaka 538B.K-1798B.K jumla Miaka 1260. 

*MFALME CONSTATINE KUONGOKA* 
Mwaka wa 321B.K, mfalme Constantine aliongoka alijiunga na kanisa..... Na Kisha akatoa Sheria kuwa watu wote katika himaya yake..waiheshimu jumapili Siku ya kupumzika ... 

*BARAZA LA LAUDIKIA*
Kisha baada ya muda, katika Baraza la Laodicea, kanisa katoliki lilipitisha Sheria ya jumapili, kukataza watu wasipumzike Siku ya sabato(jumamosi) badala yake wapumzike Siku ya kwanza ya juma (jumapili) 
Baadhi ya wakristo waaminifu walikataa kumtii mtawala na walikataa kusikiliza amri ya kanisa, na kubakia kuitunza sabato ambayo ilikuwa imeagizwa na Mungu tangu mwanzo... 

Rumi ilianza kuwatesa wale ambao walikuwa wakimtii Muumbaji na kuitunza sabato, kwa sababu ya mateso Mengi...wengi wakaamua kuitii Rumi na kuanza kuishika Siku ya jumapili Kama Siku ya ibada ....


Idadi kubwa imebakia ikitunza Siku ya jumapili ambayo ni sabato bandia.....tambua kwamba ni Shetani aliyekuwa 
Nyuma ya viongozi Hawa, ili avuruge mipango ya Mungu... ... 

*UTHIBITHISHO KUTOKA ROMA* 

Katika kitabu Cha Convert's catechism of Catholic doctrine, (1957), uk 50;  kilichoandikwa na peter Geiermann tunasoma maneno haya: 

Swali: Sabato ni Siku ipi? 
Jibu: Jumamosi ndiyo sabato 

Swali: Kwanini tunaiadhimisha jumapili badala ya jumamosi? 
Jibu: Tunaiadhimisha jumapili badala ya jumamosi kwa sababu kanisa katoliki liliuhamisha utukufu toka jumamosi Hadi jumapili. 

Hivyo, Daniel 7:25 imekwisha timia, watakatifu wa Mungu waliteswa kwa kipindi Cha Miaka 1260(nyakati 3 na nusu).
kupitia dora ya Rumi walibadili Sheria ya Nne ya Mungu, (kutoka 20:8-11) na Siku hizi waumini wa kanisa katoliki wanajua amri ya tatu sio ya Nne, kwao inasema shika kitakatifu Siku ya Bwana...tofaut na Biblia inavyosema: 

Waliondoa Sheria ya pili, usijifanyie sanamu ya kuchonga, wakabadilisha amri ya Nne...Kisha wakagawanga amri ya kumi kuziba pengo la amri ya pili, amri ya kumi ikazaa amri ya 9 na ya 10. 

*AGIZO LA MUNGU*

Sabato ni agizo la Mungu, jumapili agizo la mwanadamu, inapendeeza ukiyatenda mapenzi ya Mungu, aliyekuumba! 
Isaya 66:22-23
[22]Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 

[23]Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA. 

Sabato itakuwepo Hadi milele, hata baada ya dunia hii kuumbwa upya sabato itadumu milele yani ibada Siku ya jumamosi: 

- Let's learn together - 
Amani ya Bwana iwe Juu yako--- 

Comments

Popular posts from this blog

MTU ANAPOKUFA ANAENDA WAPI?

Mara nyingi, tumesikia hadithi nyingi kuhusu wafu, wengine wakiamini kuwa mtu anapokufa huwa anaendelea kuishi katika ulimwengu mwingine, je! Ukweli halisi ni upi??  Karibu tujifunze pamojaa kwa kuangalia maandiko yanasemaje!!  MWANADAMU ALIUMBWA Mwanadamu ni matokeo ya udongo jumlisha pumzi ya uhai,  [Mwanadamu=udongo+pumzi ya uhai] BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. (Mwanzo:2:7) Hivyo, ukichukua udongo ukatoa na pumzi ya uhai unapata maiti,  [Maiti=Udongo-pumzi ya uhai] KIFO HAUKUWA MPANGO WA MUNGU Kifo ni matokeo ya dhambi, baada ya adamu na Hawa kuvunja sheria ya Mungu, pale kwenye bustani ya Edeni[mwanzo 3:1-24] Ikiwa Kama adamu na Hawa wasingetilia Shaka maagizo ya Mungu, Leo kifo kisingekuwepo kabisaa hakuna hata mmoja ambaye angekuwa anahisi maumivu tunayohisi leoo.... (EGW, Pendo lisilo kifani, sura ya Anguko la Mwanadamu) Biblia inafananisha KIFO na usingizi, maana baada ya muda Yesu akirudi...

UHALISIA WA UWEPO WA MUNGU

 JE MUNGU YUPO KWELI?  Watu wengi wamehoji maswali Mengi ikiwa Mungu yupo au la, na baadhi wamefikia hatua ya kusema kuwa hakuna Mungu!  Swali linakuja ikiwa Mungu yupo wawezaje kuthibitisha Imani yako?  UTHIBITISHO WA  UWEPO WA MUNGU  Mungu, yupo! Upo uthibitisho tosha kujibu swali hili Kama ifuatavyo!.  1. Uwepo wa Ulimwengu huu  Vitu vinavyoonekana vyote, Kama vile mimea, wanyama, mfumo wa jua (Solar system) na sayari zingine zote, kuwepo kwake Lazima awepo mwasisi wake! Maana hakuna uthibitisho wowote unaonesha kuwa sayari yaweza jiumba yenyewe!!, Wala dhana ya uibukaji haileti mantiki kusema mfumo wa Jua ulivyokaa uliibuka tuu.  2.  Mpangilio, mwafaka na Muundo wa Ulimwengu.  Jinsi Ulimwengu ulivyo, Kuna aliyepangilia, aka design(Muundo) ili kupata rangi/mwonekano mzuri wenye kuvutia, angalia aina za mimea, maua, wanyama tofauti kwa aina zake, ndege tofauti wakivutia sana!  Jua litoke mashariki kwenda magharibi Bila kuhama...

SIKU YA SABATO NI IPI?

Wengi, wanatunza Siku ya jumapili na wengine Siku ya jumamosi... Swali linakuja je, Kati ya hizi mbili ipi ni Siku ya kweli?...  SABATO YA BWANA  Biblia inasema;  Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. [Waefeso 4:5] Kwa mujibu wa Biblia upo ubatizo mmoja(wa maji Mengi) Yuko Mungu mmoja na Imani moja.....(Siku ya ibada lazima iwe moja) Kama wakiwa na Imani moja....  SABATO NI AMRI YA NNE Katika kutoka 20:8-11 tunasoma maneno haya;  [8]Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.  [9]Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;  [10]lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.  [11]Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.  -----------------------------...