JE MUNGU YUPO KWELI?
Watu wengi wamehoji maswali Mengi ikiwa Mungu yupo au la, na baadhi wamefikia hatua ya kusema kuwa hakuna Mungu!
Swali linakuja ikiwa Mungu yupo wawezaje kuthibitisha Imani yako?
UTHIBITISHO WA UWEPO WA MUNGU
Mungu, yupo! Upo uthibitisho tosha kujibu swali hili Kama ifuatavyo!.
1. Uwepo wa Ulimwengu huu
Vitu vinavyoonekana vyote, Kama vile mimea, wanyama, mfumo wa jua (Solar system) na sayari zingine zote, kuwepo kwake Lazima awepo mwasisi wake! Maana hakuna uthibitisho wowote unaonesha kuwa sayari yaweza jiumba yenyewe!!, Wala dhana ya uibukaji haileti mantiki kusema mfumo wa Jua ulivyokaa uliibuka tuu.
2. Mpangilio, mwafaka na Muundo wa Ulimwengu.
Jinsi Ulimwengu ulivyo, Kuna aliyepangilia, aka design(Muundo) ili kupata rangi/mwonekano mzuri wenye kuvutia, angalia aina za mimea, maua, wanyama tofauti kwa aina zake, ndege tofauti wakivutia sana!
Jua litoke mashariki kwenda magharibi Bila kuhama kwenye mzunguko wake!
Uibukaji usingeweza kufanya hivi, maana vitu vilivyotenegenezwa na Binadamu vina kasoro, ila vya asili havina kasoro, hii ni kusema uibukaji/mlipuko unazidi akili Binadamu!! La,
---Hapa lazima awepo aliyekuwa asimamia na kuratibu mambo yote haya!
3. Sayansi ya uchunguzi ya jamii za wanadamu
Kila mwanadamu anajua jema na baya, hata wanyama pori pia wana Nidhamu Fulani ndani yao ya utii, walipewa na Nani,,,,,Hawa wanyama?
Uwepo wa dhamiri ndani ya mwanadamu huonesha kuwa Yupo aliyeweka hiyo dhamiri,
Dhana ya kuibuka, haiwezi kutoa dhamiri ya kujua Mema na mabaya!! maana na yenyewe haijui chochote!
4. Hulka ya Ufahamu
Kila mwanadamu kwa asili ana amini uwepo wa nguvu iliyo Juu ya uwezo wake, ndo maana kila jamii Wana mfumo wa ibada, utakuta anaabudu kitu Fulani....
--- Hii inaonesha uwepo dhahiri wa nguvu(Mungu) iliyo chimbuko letu!
5. Uthibitisho wa maandiko
Kwa kuangalia Biblia inafunua kuwa Mungu yupo, na ndiye Muumbaji wa vyote vilivyoko duniani.
Katika mwanzo sura ya 01 yote.
6. Mizani ya nguvu za kiroho
Tumeshuhudia mapepo yakitolewa!! Kwa maombi tu, Miujiza! Iliyo kinyume na nguvu za Giza, uwezo wa kufufua mtu kwa ombi tu,
Miujiza yote hiyo huashiria utendaji kazi wa nguvu kubwa zaidi(Mungu)
---Daima halikushindikana Jambo lolote Alipoitwa huyu muumbaji kwa dhati, hii huonesha kuwa yupo ndo maana anajibu maombi.
.................................
---Amani ya Bwana iwe Juu yako---- Hesabu 6:25
Ubarikiwe mtumishi
ReplyDeleteAmina...Amani ya Bwana iwe Juu yako!
DeleteGood kufundisha watu
ReplyDeleteYes! Karibu Sana....
DeleteBe blessed brethren I gained something and it will be implemented to my life
ReplyDeleteAmen, you too! May our Almighty God keep you safe!
Delete