UUMBAJI WA SAYARI YETU YA DUNIA
Dunia yetu hii na vyote vilivyomo viliumbwa na Mungu kwa muda wa siku sita. Hapa ni siku sita za masaa 24HRS, (Yome[Hebrew]- inayotafasiliwa Kama siku...inamanisha tangu jua kuzama Hadi Jua kuzama sio miaka 6,000 Kama waanavyodhani wengine. [Mwanzo 1:1]
Dunia Ina vitu vingi, ndiyo! Mimea aina tofauti, wanyama, n.k kwa Mungu haya sio Mengi kiasi Cha kushindwa kuumba kwa Siku sita tuu, alikuwa anatamka vinatokea!! Kama ifuatavyo;
-- Siku ya kwanza (01)
Siku ya kwanza Mungu aliumba *NURU* hapo ndipo mwanzo wa Giza na Nuru ulipopatikana.....
Mwanzo 1:3-5
[3]Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru...
-- Siku ya pili (02)
Siku ya pili Mungu aliumba *ANGA*
Mwanzo 1:6-8
[6 ]Mungua akasema Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji....
-- Siku ya tatu (03)
Siku ya tatu Mungu aliumba, *NCHI KAVU* *BAHARI* na *MIMEA*
Mwanzo 1:9-11
[9]Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.
[10]Mungu akapaita pale pakavu nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
[11]Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
-- Siku ya Nne (04)
Siku ya Nne Mungu aliumba *JUA* *MWEZI* na *NYOTA*
Mwanzo 1:14-19
[16]Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.
-- Siku ya tano (05)
Siku ya tano Mungu aliumba *VIUMBE WA MAJINI* na *NDEGE WA ANGANI*
Mwanzo 1:20-23
[20]Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.
-- Siku ya Sita (06)
Siku ya mwisho(06) Mungu aliumba *WANYAMA WOTE* na akamalizia kwa kumuumba *MWANADAMU*
Mwanzo 1:24-31
[24]Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
-------------------------------
-------------------------------
Binadamu Ndiye kiumbe pekee aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu,
Mwanadamu alipotoka mikononi mwa Mungu alikuwa mkamilifu, Bila dosari... Ndani yake akiwa na tabia halisi ya Mungu!!
Kila kitu kilichoumbwa na MUNGU, kilikuwa chema!
Mwanzo 1:31
Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita...
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Leo, dunia imeharibika, ubora umepotea, dunia Imekuwa Tena haitamaniki, nini kilichotekea mpaka dunia Imekuwa hivi?
----------------------------------
Endelea kufatilia, masomo yanayofuata tutajifunza!! Nini kilitokea!
---- Amani ya Bwana iwe Juu yako---- Hesabu 6:25
Good work composure
ReplyDeleteAlright, we thank you for good feedback, keep visiting our blog for more lessons!
Delete