Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2025

KUZALIWA MARA YA PILI

SoMo lililopita tuliona kuwa ukimwamini Yesu, ukatubu utasamehewa dhambi, hata Kama zilikuwa nyingi kiasi gani....upendo mkuu ajabu! Kiroho mtu aweza kuzaliwa Mara ya pili kwa njia ya ubatizo!......  Kwa njia ya ubatizo, mtu atamkiri Yesu, kuwa ni mwokozi wake, ndiyo njia Mungu aliyoiweka ya kutuvusha kutoka mahali pa dhambi, kutuunganisha na Mwokozi, kwa kufanya tendo hili...inakuwa umemkubali Yesu waziwazi.... hivyo, baada ya kubatizwa atakupokea, Kama mtoto wake!....nawe utakuwa umeanza safari mpya ya maisha!  UBATIZO Je, mtu anayebatizwa anapaswa awe na sifa gani?  Biblia inasema:  Marko 16:15-16 [15]Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.  [16]Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.  Kutoka kwenye Aya hii tunapata Mambo 3.  a) Injili  Kabla mtu hajabatizwa lazima ajue kweli (Neno la Mungu), ili aelewe anabatizwa kwa sababu gani!.  b)Imani  Baada ya kuhubiriwa, na kuitikia sauti ya ...

UZOEFU WA WOKOVU

Uzoefu wa wokovu hujumuisha kutubu, kuungama, msamaha, kuhesabiwa haki na kutakaswa.  Mchakato huu huanza baada ya mwanadamu aliyeanguka dhambini kusikia wito ndani yake, ambao kimsingi ni sauti ya Roho mtakatifu inayonong'ona ndani yake, hivyo huanza kutambua dhambi yake na kuijutia.... ikiwa atakubali wito huo, hufanya uamuzi wa kufata hatua hizi, kutubu, kuungama , msamaha, kuhesabiwa haki na hatimaye hupata utakaso!![Matendo 2:37-38]  1.KUTUBU(TOBA)  Neno *kutubu / toba*, hutokana na neno la Kiebrania *nachum* lenye maana ya kuhuzunika, kusikitika.  Neno la Kigiriki lenye maana sawa na hilo ni *metanoeo*, lenye maaana ya kubadilisha mawazo/nia- Hivyo, aliyetenda dhambi baada ya kutambua dhambi yake, husikitika kwa kufanya hivyo, Kisha hunuia kuiacha! Na kubadilisha mwelekeo wake! Huku ndiko kutubu!!  2. KUUNGAMA  Kuungama ni kukiri au kukubali Jambo wazi wazi Bila kusema uongo!  Aliyetenda dhambi baada ya kugundua kosa lake, hatua ya pili ni kuunga...

SULUHISHO BAADA YA ANGUKO

 HUZUNI ILIJAZA MBINGU Huzuni iliijaza mbingu, pale wote walipotambua kuwa wanadamu walikuwa wamepotea na dunia ambayo Mungu alikuwa ameiumba ilikuwa ijazwe na wanadamu wapatikanao na mauti wanaopitia maisha ya taabu, maradhi, na mauti, pasipo na njia ya kuokoka kwa mkosaji. Familia yote ya Adamu ni lazima wafe. - EGW, PLK 26.1 MPANGO WA KUMKOMBOA MWANADAMU  Ndipo Yesu akawafahamisha jeshi la malaika kwamba njia ya kuokoka ilikwisha kupatikana kwa ajili ya wanadamu waliopotea. - EGW, PLK 26.2 Aliwaambia kuwa alikuwa amemsihi Baba yake kwamba Yesu ajitolee maisha yake kuwa fidia ya kuwakomboa - EGW, PLK 26.2 Angetumikia adhabu ya kifo juu yake mwenyewe, ili kwa kupitia kwake wanadamu waweze kupata msamaha. -  EGW,PLK 26.2 YESU KATIKA UMBO LA BINADAMU Angeacha utukufu wake wote mbinguni, na kutokea duniani kama mwanadamu, kujinyenyekesha kama mwanadamu, kupitia uzoefu wake mwenyewe ajue majaribu mbalimbali ambayo yangewapata wanadamu, ili apate kujua jinsi ya kuwasaidia w...