Hili limekuwa swali kuu, kwanini idadi kubwa ya watu wanashika Siku ya kwanza(01) ya juma yaani jumapili Kama Siku ya ibada? Katika Somo la Siku ya sabato ni ipi tumejifunza, kuwa sabato ya kweli ni jumamos: Ikiwa ndivyo, jumapili iliingiaje Kama Siku ya ibada, hadi wengi wanaishika leoo...karibu tujifunze pamoja.... *YESU ALITUNZA SABATO* Katika kitabu Cha Luka 4:16 anasema: ilikuwa desturi ya Mwokozi kusali Siku ya sabato(jumamosi) kumbe Yesu hakutunza jumapili Kama Siku ya ibada .... *MITUME WALITUNZA SABATO* Katika kitabu Cha matendo 16:13 neno linasema: Mitume hata baada ya Yesu kupaa mbinguni bado waliendelea kutunza sabato .....kamwe hawakushika jumapili, maana ilikuwa Siku ya kazi. *BADILIKO LA SABATO, LILITABIRIWA KWENYE MAANDIKO Katika kitabu Cha Daniel 7:25 inasema: [25]Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wa...
Mara nyingi, tumesikia hadithi nyingi kuhusu wafu, wengine wakiamini kuwa mtu anapokufa huwa anaendelea kuishi katika ulimwengu mwingine, je! Ukweli halisi ni upi?? Karibu tujifunze pamojaa kwa kuangalia maandiko yanasemaje!! MWANADAMU ALIUMBWA Mwanadamu ni matokeo ya udongo jumlisha pumzi ya uhai, [Mwanadamu=udongo+pumzi ya uhai] BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. (Mwanzo:2:7) Hivyo, ukichukua udongo ukatoa na pumzi ya uhai unapata maiti, [Maiti=Udongo-pumzi ya uhai] KIFO HAUKUWA MPANGO WA MUNGU Kifo ni matokeo ya dhambi, baada ya adamu na Hawa kuvunja sheria ya Mungu, pale kwenye bustani ya Edeni[mwanzo 3:1-24] Ikiwa Kama adamu na Hawa wasingetilia Shaka maagizo ya Mungu, Leo kifo kisingekuwepo kabisaa hakuna hata mmoja ambaye angekuwa anahisi maumivu tunayohisi leoo.... (EGW, Pendo lisilo kifani, sura ya Anguko la Mwanadamu) Biblia inafananisha KIFO na usingizi, maana baada ya muda Yesu akirudi...